Maskani Wikendi Okt, 5-6, 2024


SEHEMU YA 1: MASKANI KWA APOLLO WIKI HII

Yaliyojiri

Jumatatu: Hapo jana, kijana wa mtaa, Moyale Mishale, alipiga mzinga! Kijana huyu wa Apollo Veve Baze, alimuonesha pwagu mmoja kilichomtoa kanga manyoya alipojaribu kutoroka na suruali ya Sh1500 baada ya kununua t-shirt na kofia. Moyale alimtia kibindoni mwizi huyo kwa mbinu za kijeshi – yes, zile za TV tu! Alichomoa uaminifu wake kwa mwajiri wake, akakataa hongo ya Sh500.

Jumanne: Jana ilikuwa furaha tu, Apollo Veve Baze lilijaa shangwe na vigelegele baada ya Apollo mwenyewe kutimiza ahadi yake ya kuanza kuzawadi Wanabaze  jaba la Sh50! Kama umeikosa, basi umezubaa! Jaba hilo la bure linapatikana Jumatatu, Jumanne, na Alhamisi, lakini kuna twist — sharti uwe MwanaBaze Wa Leo ili upate bonge hilo la jaba. Si ajabu, kila mtu sasa anataka kuwa featured kwenye Maskani Leo! Na si kawaida, ndio maana leo ilikuwa siku ya zawadi na zawadi iliruka kama ndege!

Jumatano: Siku ilikuwa ya hali ya utulivu mjini Gatura. Boda boda hazikuongeza kasi, na hata upepo ulionekana kupumzika, lakini kule kwa Apollo Veve Baze mambo yalikuwa tofauti kabisa! Mauzo ya jaba yalichomoka kama jua la mchana; hadi kufikia saa kumi na mbili, kila kitu kilikuwa kimeshaenda. WanaBaze waliojifanya watatulia hadi jioni, walikuta jaba limeisha. Ah! Rekodi za mauzo zilibadilika, na historia mpya ikaandikwa!

Alhamisi: Kila mtu anajua Jumatano ni siku ya kazi na soko Gatura, lakini Apollo Veve Baze ikawa kama kanisa la harusi! WanaBaze walijaa hadi capacity! Ungefikiri wameitisha sherehe ya kijiji. Hata sehemu ya nje pale kwenye fresh air na zile viti za ku enjoy space, kila kiti kilikuwa kimenyakuliwa. Kufikia saa nane, Baze ilikuwa full capacity, na kila mtu alionekana akiburudika huku wakifurahia ile mali safi ya Apollo!

Ijumaa: Alhamisi haikubaki nyuma! WanaBaze walikumbuka maisha ya zamani wakikumbatiana na 'Tbt' — zile siku ambapo walipiga sherehe bila story za bundles au pressure ya 'soft life.' Ilikuwa raha tupu, na mbwembwe za zamani zilirudi upya! Apollo Veve Baze ilikuwa moto ile mbaya, hadi midundo ya nyimbo za zamani zilipigwa ili kuongeza ladha ya kumbukumbu za good old days!

Kaeni chonjo kwa wiki ijayo, maana mambo yatanoga zaidi! Hadi basi, safari ya Apollo Veve Baze inaendelea... Wikendi njema!

SEHEMU YA 2: HABARI MSETO

Ruto alivyoibuka mfalme wa abautani, leo hiki kesho kile – Taifa Leo

RAIS William Ruto amejitokeza kama bingwa wa kwenda kinyume na kauli alizotoa kuelekea uchaguzi mkuu uliopita na hata miaka miwili baada ya kuingia afisini, hali inayomfanya kuonekana kama kiongozi asiye na msimamo thabiti.

Dkt Ruto amejikanganya kuhusiana na sera anazotoa akiwa mamlakani, wakati mwingine akifanya hivyo miezi miwili baada ya kuzitoa, na hivyo msimamo wake kutiliwa shaka.

Kufikia sasa Rais amejikanganya kuhusu shughuli za Wakfu wa Ford nchini, kudhulumiwa kisiasa kwa naibu wake Rigathi Gachagua, madai ya kutekewa nyara kwa wakosoaji wa serikali yake ya Kenya Kwanza, ukiukaji wa maagizo ya mahakama, kuwaingiza serikalini viongozi wa upinzani miongoni mwa mambo mengine aliyoapa kutoruhusu kufanyika wakati wa utawala wake.

Wakati huu Bw Gachagua anakabiliwa na vitisho vya kung’olewa mamlakani kupitia hoja inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni na wandani wa Dkt Ruto.

Naibu Rais pia amelalamika kuwa anahujumiwa kimakusudi na maafisa wa ngazi za chini serikalini. Aidha, Bw Gachagua amedai asasi za usalama zinatumika kumtisha pamoja na wandani wake.

“Matumizi ya maafisa wa asasi za usalama kama silaha katika vita vya kisiasa ni mbinu iliyopitwa na wakati. Rais Ruto na mimi, baada ya kuingia afisini, tuliwaahidi Wakenya kwamba maafisa wa usalama hawatatumiwa katika vita vya kisiasa. Naaibika kuwa tumerejelea tulipokuwa zamani,” Bw Gachagua akasema Alhamisi.

Alidai kuna mipango ya kuwawekelea mashtaka bandia wafanyakazi watatu katika afisi yake na wandani wake, Mbunge wa Embakasi Kaskazini James Gakuya na Benjamin Gathiru (Embakasi ya Kati).

Wakati wa kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022, Dkt Ruto aliapa kutoruhusu naibu wake kupitia mateso aliyopita baada ya kutofautiana na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

“Sitaruhusu Naibu Rais chini ya utawala wangu kuteswa namna makamu wa raia wa zamani waliteswa na jinsi nimekuwa nikidhulumiwa na kukosewa heshima,” akasema.

Kwenye mahojiano mengine katika runinga ya NTV, Dkt Ruto alisema hivi: “Nataka kukuambia kwamba haitatendeka. Nataka nikwambie kuwa sitaruhusu naibu wangu adhulumiwe na wafanyakazi wa vyeo vya chini”.

Vile vile, wiki hii akiwa jijini New York Amerika Rais Ruto alimiminia sifa Wakfu wa Ford kwa mchango wake katika ukuzaji demokrasia nchini Kenya kupitia ufadhili wake.

Lakini miezi miwili iliyopita alisuta wakfu huo kwa kufadhili maandamano ya vijana wa Gen Z yaliyomlazimu kuondoa Mswada wa Fedha na kisha kuwafuta mawaziri wake 21.

“Kenya inathamini zaidi kujitolea kwa Wakfu wa Ford katika kukuza demokrasia yetu na kuunga mkono harakati za Kenya za kutaka mageuzi katika asasi za kiuchumi ulimwenguni, mikakati ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na teknolojia ya kisasa. Nilifanya mazungumzo na Rais wa Wakfu wa Ford Darren Walker jijini New York,” Dkt Ruto akasema Jumanne kupitia ukurasa wake wa mtandano wa X.

Lakini mnamo Julai mwaka huu, Dkt Ruto alidai wakfu huo ulihusika katika visa vya kusababisha machafuko na kuvuruga mafanikio ambayo Kenya imefikia katika mawanda ya kidemokrasia.

“Tunataka Wakfu wa Ford uelezee Wakenya mchango wake katika maandamano ya juzi. Tutawashutumu wale wote wanaolenga kuhujumu demokrasia yetu tuliopata baada ya mapambano makali,” Rais Ruto akasema kwenye mkutano wa hadhara katika eneo la Keringet, kaunti ya Nakuru.

Baadaye Katibu wa Wizara ya Masuala ya Kigeni Korir Sing’oei aliandikia wakfu huo akiutaka kuelekeza jinsi misaada yake kwa mashirika mbalimbali ya kijamii nchini inavyotumika.

Dkt Sing’oei alidai kuwa mashirika ambayo hupokea ufadhili kutoka kwa wakfu huo ndiyo yalipanga maandamano ya kupinga serikali na kuiondoa mamlakani.

“Mazoea ya Dkt Ruto ya kubadili misimamo yanamsawiri kama kiongozi asiyetabirika, zilivyo sera za serikali,” anasema Profesa David Monda, mhadhiri na mchanganuzi wa masuala ya kisiasa.

Baada ya kuwafuta kazi mawaziri wake 21 Julai 8, mwaka huu Rais Ruto aliamua kuteua viongozi wakuu watano wa ODM katika baraza jipya alilobuni.

Wao ni; Mr Opiyo Wandayi (Waziri wa Kawi na Mafuta), John Mbadi (Fedha), Hassan Joho (Uchimbaji Madini na Uchumi wa Majini), Wycliffe Oparanya (Vyama vya Ushirika) na Beatrice Askul (Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki).

Lakini Dkt Ruto alitetea hatua hiyo, akifahamu kuwa ni kinyume cha ahadi yake kabla ya uchaguzi wa 2022, akisema ililenga kupalalia umoja nchini na kufanikisha shughuli za maendeleo. 

Wasiwasi kuhusu mabadiliko serikalini iwapo ‘mwenye hisa’ Gachagua atatimuliwa – Daily Nation

WASIWASI umekumba maafisa wakuu katika utawala wa Rais William Ruto kuhusu uwezekano wake kufanywa mabadiliko serikalini baada ya Naibu Rais Rigathi Gachagua kutimuliwa.

Duru zinasema kuwa mabadiliko hayo yanaweza kufanyika hata katika uongozi bungeni na uongozi wa kamati mbalimbali.

Mabadiliko bunge yatafanywa kwa misingi ya nafasi ya baadhi ya wabunge katika mchakato wa kuondolewa kwa Gachagua kwani huenda wandani wake wakaathirika pakubwa.

Katika Serikali Kuu, huenda Rais akafanya mabadiliko katika Makatibu wa Wizara ili kuendeleza masilahi ya wandani wapya akiwemo Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga.

Mnamo Julai mwaka huu, Rais Ruto aliwafuta kazi mawaziri wake 21 kutimiza matakwa ya vijana wa Gen Z waliofanya msururu wa maandamano kupinga serikali yake.

Alishirikisha wandani wa Bw Odinga katika baraza jipya la mawaziri aliloliunda.

Inaaminika kuwa Bw Gachagua alikuwa na ushawishi mkubwa katika teuzi kuu serikali tangu Dkt Ruto alipoingia mamlakani mnamo Septemba 2022.

Baadhi ya wale ambao alishawishi uteuzi wao huenda wangali waaminifu kwake, hali ambayo huenda ikiwagharimu pakubwa endapo Gachagua atatimuliwa.

Katibu Mratibu wa UDA Vincent Musyoka (Mbunge wa Mwala) aliambia Taifa Leo kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa Rais Ruto atafanya mabadiliko serikalini.

Alisema hatua ya kwanza itakuwa ni kumteua yule atakayejaza nafasi ya Gachagua, endapo atatimuliwa.

Hata hivyo, alisema wale wanaoshikilia nyadhifa zingine kuu watawekwa katika mizani kwa misingi ya utendakazai wao sio kwa misingi ya yule aliyewasilisha majina yao ili wateuliwe.

“Mabadiliko serikalini yataanza na kujazwa kwa nafasi ya Gachagua. Nakuambia kuwa Rais ni mtu ambaye anaweza kufanya mambo ya kushtua. Ikiwa wewe ni waziri au katibu wa wizara na unafanya kazi yako vizuri bila kuhujumu serikali kutoka ndani, uhusiano wako na mtu mwingine hauwezi kutumika kama msingi wa kukubadilisha au kukufuta kazi,” akasema Bw Musyoka, almaarufu Kawaya.

“Rais Ruto anawaelewa zaidi maafisa wake. Utashangaa kupata kwamba yule ambaye jina lake liliwasilishwa na mtu mwingine anayo uhusiano wa karibu zaidi naye,” akaeleza Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Kawi.

KIPANYA

HITIMISHO

Mchapishaji Paul Kimani

Mhariri: askMRMOI

© Maskani Leo ni Chapisho la Apollo Veve Baze, 2024.